Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, anaripotiwa kuwa tayari kwa wazo la kujiunga na Liverpool msimu ujao huku akitafuta njia ya kuondoka Paris St-Germain 2024. (L'Equipe - kwa Kifaransa, usajili unahitajika)
Manchester City inamfuatilia mshambuliaji wa Brighton Evan Ferguson, 18, ambaye mchezo wake uko katika kiwango cha juu, kwa imani mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Ireland anaweza kucheza pamoja na Erling Haaland. (inews)
Manchester United wameanza kujadili mkataba wa beki wao Aaron Wan-Bissaka baada ya utendakazi wa Muingereza huyo, 25, kumvutia kocha Erik ten Hag mwaka huu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Liverpool walikuwa tayari kubadilishana mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 24, kwa winga wa Ureno Joao Felix msimu huu lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwapuuza Reds, Manchester United na Aston Villa kulazimisha uhamisho wa mkopo kwenda Barcelona kutoka kwa wapinzani wa La Liga Atletico Madrid. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Wazabuni wawili wakuu katika kinyang'anyiro cha kutwaa Manchester United wanasema hawajaambiwa klabu hiyo itaondolewa sokoni licha ya kushuka kwa bei ya hisa ya Mashetani Wekundu kwa pauni milioni 600. (Mail)
Mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Raheem Sterling, 28, hatastaafu kucheza soka ya kimataifa licha ya kuachwa tena kwenye kikosi cha Three Lions cha Gareth Southgate. (Telegraph - usajili unahitajika)
Winga wa Everton na Jamaica Demarai Gray, 27, anatarajiwa kuondoka Goodison Park ili kutia saini mkataba wa miaka minne na klabu ya Al-Ettifaq ya Saudi Pro League, inayonolewa na gwiji wa Liverpool Steven Gerrard. (Fabrizio Romano)
West Ham wamejiunga na Uturuki Galatasaray na Fenerbahce katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungocwa zamani wa Manchester United na England Jesse Lingard mwenye umri wa miaka 30. (Football Insider)
Kiungo wa Denmark Jesper Lindstrom, 23, alikataa uhamisho wa £25m kutoka Eintracht Frankfurt kwenda Liverpool na badala yake akajiunga na Napoli kwa sababu atapata muda zaidi wa kucheza na mabingwa hao wa Serie A. (Tipsbladet- Danish)
Chelsea wanamtaka beki wa pembeni Ian Maatsen kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Stamford Bridge baada ya Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 21 kukataa uhamisho wa pauni milioni 31 wa klabu ya zamani ya Burnley kwa mkopo siku ya mwisho. (Fabrizio Romano)
Wakala wa Jorginho anasema kuwa kiungo huyo wa kati wa Italia, 31, atasalia Arsenal licha ya kumtaka Fenerbahce katika Ligi Kuu ya Uturuki, ambapo dirisha la uhamisho litaendelea kuwa wazi hadi Septemba 15. (Tutto Mercato - kwa Kiitaliano)
Mfaransa Christophe Galtier, 57, aliyefutwa kazi na Paris St-Germain mwezi Julai licha ya kushinda taji la Ligue 1, anatarajiwa kurejea kwenye uongozi kwa kuchukua nafasi ya Hernan Crespo kama bosi wa klabu ya Al-Duhail ya Qatar. (RMC Sport - kwa Kifaransa)
BBC



