Klabu ya Azam Fc imemrejesha kiungo mkabaji Samwel Onditi aaliyekuwa akikipiga kwa mkopo Geita Gold
Benchi la ufundi la Azam Fc chini ya kocha Dabo, limependekeza kurejeshwa kwa kiungo huyo ili kuimarisha safu ya kiungo
Onditi anatarajiwa kusaini mkataba wa muda mrefu zaidi
Azam Fc imekuwa ikiandamwa sana na majeraha kwa wachezaji wao wanaotumikia eneo la kiungo
Walimsajili Yannick Bangala kutoka klabu ya Yanga lakini nyota huyo akaumia mara baada ya kujiunga nao
Licha ya kurejea kikosini bado hana utimamu wa kucheza dakika 90
Saospeter Bajana ni kiungo mwingine tegemeo ambaye pia alipata majeraha na kukosekana katika mechi ya mkondo wa pili kuwania kufuzu raundi ya kwanza ya CAF CC dhidi Fasil Kenema na Ethiopia Azam Fc ikitupwa nje kupitia mikwaju ya penati



