Simba - Local

Kramo, Miquissone waongeza matumaini Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Sep 2023
Kramo, Miquissone waongeza matumaini Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema ubora wa Luis Miquissone na Aubin Kramo unamuongezea upana wa kikosi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na African Football League

Akizungumza maendelea ya wachezaji hao baada ya kucheza mechi mbili za kirafiki, Robertinho amesema nyota hao wameendelea kuimarika na wanampa matumaini kuelekea mechi muhimu za ligi ya mabingwa na African Football League

"Nimewapa nafasi wachezaji wote ili kuona uwezo wa kila mmoja. Nafurahi kuona Miquissone ameanza kuonyesha uwezo mzuri, amecheza kwa dakika zote 90 na ameonyesha kiwango bora"

"Kwa upande wa Kramo licha ya kuingia kipindi cha pili kwenye mechi zote mbili za kirafiki, pia amenipa kitu kikubwa akifunga mabao mawili. Nitaendelea kumpa nafasi zaidi ili kuwa bora zaidi ya alipo sasa"

"Ni mchezaji mzuri lakini bado naendelea kumpa muda zaidi ili apate uzoefu wa ligi ya Tanzania. Tayari nimeanza kumpa dakika chache kwenye mechi za kirafiki na ameonyesha uwezo mkubwa kwani ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na naamini watatusaidia," alisema Robertinho

Simba inaendelea na mazoezi Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Power Dynamo

Mchezo huo utapigwa Septemba 16 katika uwanja wa Levy Mwanawasa huko Zambia

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
39m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
52m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’