Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' saa 4:00 usiku leo itakuwa katika uwanja wa 19 May 1956 (Annaba) kucheza mechi ya mwisho hatua ya makundi kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Algeria
Stars inashika nafasi ya pili katika kundi E ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Uganda yenye pointi nne
Katika mchezo huo Stars inahitaji matokeo ya sare au ushindi ili kujihakikishia tiketi ya kucheza Afcon 2023 kwa mara ya tatu katika historia yake
Pia dua za Watanzania ni kuona Uganda haipati ushindi katika mechi yao dhidi ya Niger leo saa 4:00 usiku ugenini, kwani ni matokeo ambayo yataihakikishia Tanzania kwenda Afcon 2023 hata kama itafungwa na Algeria
Stars ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho jana, wachezaji wako tayari kwa mchezo huo muhimu siku ya leo