Transfer - International

Tetesi za usajili Jumamosi, Septemba 09 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Sep 2023
Tetesi za usajili Jumamosi, Septemba 09 2023

Newcastle United wamepiga hatua katika mazungumzo ya kurefusha mkataba wa kiungo wa Brazil Bruno Guimaraes, 25, na makubaliano sasa yanaribia kufikiwa. (Fabrizio Romano)

Chelsea na Manchester City zilnamfuatilia Guimaraes, ambaye mkataba wake wa Newcastle utaendelea hadi 2026, msimu huu wa joto. (90 min)

Rangers wamemtaja mkufunzi wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter kama mbadala wa kocha wa sasa Michael Beale. (Football Insider)

Arsenal na Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia winga wa Brugge kutoka Norway Antonio Nusa, 18, ambaye alikataa nafasi ya kujiunga na Chelsea mwishoni mwa dirisha la usajili. (90mi)

Kukosa muda wa kucheza Aston Villa kunamkwaza iiungo wa Ubelgiji Youri Tielemans, 26, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa uhamisho wa bure msimu uliopita baada ya kandarasi yake Leicester City kuisha. (Goal) Brighton wanapania kumsajili winga wa Japan Kaoru Mitoma mwenye umri wa miaka 26 kwa kandarasi mpya ifikapo mwisho wa mwaka. (90 min)

Manchester United ingependa kumtoa kiungo wa kimaifa wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa nchini Uturuki wiki ijayo. (Football Insider)

Chelsea iliingilia kati kuzuia Wolves kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Habib Diarra, 19, kutoka klabu dada yao Strasbourg msimu huu. (Football Insider)

Mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Andy Carroll, 34, anasema alikuwa na ofa ya kusalia Uingereza kabla ya kuamua kujiunga na Amiens inayoshiriki Ligi ya Ufaransa ya Ligue 2. (Sun)

Kiungo wa Chelsea Romeo Lavia, 19, amepata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mazoezi na klabu hiyo inasubiri matokeo ya uchunguzi ili kubaini ukubwa wa suala hilo kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Guardian)

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, anakabiliwa na kibarua kigumu cha kupata uungwaji mkono wa wachezaji wenzake wa Manchester United, pamoja na kocha Erik ten Hag, kufuatia mwenendo wake baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Arsenal. (ESPN)

Manchester City iliwasiliana na Barcelona kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania Alejandro Balde, 19. (Fabrizio Romano, via Sport - kwa Kihispania)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’