Klabu ya Yanga leo Jumamosi ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kiluvya United inayoshiriki League One
Wananchi wameibuka na ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Avic Town
Washambuliaji Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni kila mmoja alifunga mabao mawili huku Farid Mussa na Crispine Ngushi nao wakipachika mabao
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe aliwapongeza Kiluvya United kuwa na ujasiri wa kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga
Mapema wiki hii Kamwe alitangaza kuikaribisha timu yoyote nchini kucheza mechi ta kirafiki dhidi ya kikosi chao ambacho kinajiandaa na mchezo wa kuwania tiketi ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Mereikh
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 16 huko Rwanda