Real Madrid wanalenga kumnunua mlinzi wa Bayern Munich Alphonso Davies, 22, msimu ujao wa joto. (Marca In Spanish)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumnunua mlinzi wa West Ham na Morocco Nayef Aguerd msimu ujao, lakini atakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester City kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sun)
Meneja wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekataa nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya wanawake ya Norway. (Mirror)
Chelsea, Barcelona na Bayern Munich zote zilijaribu kumsajili Marco Verratti, 30, kutoka Paris Saint-Germain msimu huu wa joto. (Football Transfers)
Kiungo huyo wa kati wa Italia sasa anatazamiwa kujiunga na Al Arabi ya Qatar kutoka PSG kwa euro 45m (£38.7m). (Fabrizio Romano)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anatazamiwa kuzungumza na Jadon Sancho siku ya Jumatatu kwa mara ya kwanza tangu meneja huyo amshutumu winga huyo wa Uingereza kwa kutofanya vya kutosha kustahili nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo. (Telegraph – Subscriptiopn Required)
Tottenham wako mbioni kumsajili beki wa Croatia, Hajduk Split Luka Vuskovic, ambaye alikuwa akihusishwa na kuhamia Liverpool, Chelsea, PSG na Manchester City, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 hatajiunga na Spurs hadi msimu wa joto wa 2025. (Standard)
Kocha wa Barcelona Xavi anatazamiwa kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo wiki hii. (Fabrizio Romano) Aston Villa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Alex Baena, 22, kutoka klabu ya zamani ya meneja Unai Emery Villarreal. (Fichajes – In Spanish)
Inter Milan ilikataa ombi la Chelsea, Liverpool na Newcastle United kwa kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaweza kupatikana kwa takriban pauni milioni 77 mwaka ujao. (CaughtOffside)
BBC



