Msafara wa kikosi cha Simba unatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi Septemba 14 kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Jumamosi, Septemba 16, saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania) Simba itashuka uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia kuikabili Power Dynamos
Mratibu wa Simba Abbas Ally, amesema kikosi kinatarajiwa kuondoka Tanzania asubuhi kuekea Zambia ikiwa ni safari ya takribani masaa 5
Aidha msafara wa mashabiki pia utaondoka siku hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally akibainisha kuwa kutakuwa na mabasi makubwa mawili ambayo yatabeba mashabiki kuwapeleka Zambia
Simba inakwenda Zambia kusaka ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi