Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefichua mikakati ya uongozi wa timu hiyo katika kuhakikisha msimu huu wanafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya kukosa kushiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa takribani miaka 24, Yanga imepania kumaliza ukame huo
Wananchi watasafiri nchini Rwanda kuikabili Al Merrikh mchezo wa mkondo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa Jumamosi, Septemba 16 uwanja wa Pele, Kigali Rwanda
Baada ya kutumia takribani Tsh Bilioni 1.2 za bonus katika michuano ya Kimataifa msimu uliopita, msimu huu wachezaji wa Yanga wataoga mamilioni zaidi kama watafanikisha malengo ya klabu
"Msimu uliopita Yanga ilitumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya posho za wachezaji katika michuano ya kimataifa na msimu huu pia zitatumika pesa nyingi"
"Malengo ni kuhakikisha kuwa tunafanya vyema katika michuano hii ya kimataifa ili tuweze kufika mbali, malengo yetu ni kufika hatua ya makundi na lazima wachezaji wapewe posho nzuri katika kila hatua ambayo wataweza kuvuka, huo umekuwa ni utamaduni wetu"
"Timu kubwa hutumia pesa nyingi sana kwa kuwa wanao msuli mkubwa wa pesa hivyo na sisi ni wakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunatumia mbinu nzuri za kufanya vyema zaidi," alisema Kamwe