Tetesi za usajili Alhamisi, Septemba 14 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Sep 2023
Tetesi za usajili Alhamisi, Septemba 14 2023

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Brentford ya Uingereza Ivan Toney, ambaye anatumikia marufuku ya miezi minane kwa kukiuka sheria za kamari za Shirikisho la Soka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 haruhusiwi kucheza hadi tarehe 17 Januari 2024, lakini anaweza kurejea mazoezini wikendi hii. (football.london)

Juventus wanampanga kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 30, kama mbadala wa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 30, ambaye kandarasi yake inaweza kusitishwa ikiwa atabainika kukiuka sheria za kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli. (La Repubblica – in Italy)

Beki wa Manchester United na England Harry Maguire, 30, alikuwa "karibu sana" kujiunga na West Ham kwa mkataba wa pauni milioni 30 msimu huu, anasema kocha wa Hammers Kevin Nolan. (Sport)

Beki wa zamani wa Liverpool na Uingereza Glen Johnson anasema hatashangaa iwapo Mohamed Salah, 31, ataondoka Anfield na kuelekea Saudi Arabia. Liverpool ilikataa dau la pauni milioni 150 kutoka kwa klabu ya Saudi Pro League ya Al-Ittihad mwezi huu. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa zamani wa Nottingham Forest na Uingereza Jonjo Shelvey, 31, anakaribia kujiunga na klabu ya Uturuki ya Rizespor kabla ya tarehe ya mwisho ya Ijumaa. Shelvey alijiunga tu na Forest kutoka Newcastle kwa kandarasi ya miaka miwili na nusu mwishoni mwa Januari. Wakati huohuo, fowadi wa Forest wa Nigeria Emmanuel Dennis, 25, pia anakaribia kuondoka katika klabu hiyo. (Telegraph – Subscription Required)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, 56, amekataa kuwa kocha wa Ujerumani kufuatia kutimuliwa kwa Hansi Flick. Mjerumani Klopp, 56, amekuwa akiinoa Anfield tangu 2015. (Sportschau)

Vilabu nchini Uturuki na Qatar vinapigiwa upatu huku Manchester United ikitafuta kumuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26. (90min)

Hata hivyo, sasa inaonekana huenda mchezaji wa zamani wa Ajax Van de Beek atasalia Old Trafford hadi Januari. (Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uturuki Hannibal Mejbri, 20, anasakwa kwa mkopo na Besiktas. Dirisha la uhamisho nchini Uturuki linafungwa siku ya Ijumaa. (Mirror) Winga wa zamani wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard anafikiria kustaafu akiwa na umri wa miaka 32 baada ya kuachiliwa na Real Madrid. (CaughtOffside – Subscriptionn Required)

Bosi wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter, 48, ameripotiwa kukataa kuifundisha Lyon ya Ufaransa na Rangers ya Scotland. (Sun)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
51m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’