Yanga - Local

Yanga yasaka rekodi Rwanda

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Sep 2023
Yanga yasaka rekodi Rwanda

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wako nchini Rwanda wakikabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutunga hatua ya makundi, utapigwa kwenye uwanja wa Pele, Kigali saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania)

Ikisafiri na idadi kubwa ya mashabiki kutoka Tanzania, Yanga leo inaanza mkakati wa kuiondosha Al Merrikh katika michuano hiyo na kutinga hatua ya makundi

Ni takribani miaka 24 Yanga haijacheza hatua ya makundi, kikosi cha Kocha Miguel Gamondi kinasaka rekodi ya kuwarejesha Wananchi katika hatua hiyo baada ya muda mrefu

Msimu uliopita Yanga ilipata mafanikio makubwa katika michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC) ikicheza hatua ya fainali na kuvaa medali ya ushindi wa pili

Msiimu huu Yanga imejiwekea malengo ya kutinga hatua ya makundi, uongozi wa timu hiyo ukiamini kama watafanikisha malengo hayo, watakuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika hatua itakayofuata

Yanga itashuka uwanjani leo kuikabili Al Merrikh ikiwa na kikosi chake kamili

Ni mchezaji mmoja tu, nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye hakusafiri Rwanda kutokana na matatizo ya kifamilia

Baada ya kuanza vyema mechi za hatua ya awali, matarajio ya Wananchi ni kuona timu yao ikiendeleza ubabe katika mchezo huo dhidi ya Al Merrikh

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
2h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
2h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
6h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
10h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
11h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
11h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
12h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
13h ago
READ MORE β†’