Simba - Local

Ahmed atamba, Simba itamaliza Power Dynamos Dar

Joel JJ By Joel JJ
17 Sep 2023
Ahmed atamba, Simba itamaliza Power Dynamos Dar

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos, kikosi kinarejea nchini kujipanga na mchezo wa marudiano ambao utapigwa Oktoba mosi nchini Tanzania

Ahmed amesema walitarajia mchezo huo kuwa na ushindani kwa kuwa Power Dynamos sio timu nyepesi, wakiwa mabingwa wa ligi kuu ya Zambia

"Tulitarajia mchezo hautakuwa mwepesi, mchezo huu umetupa kipimo sahihi cha mechi ya ligi ya mabingwa. Hatukuwa vizuri sana kwenye kipindi cha kwanza, lakini unaona tulirejea tukiwa imara zaidi kwenye kipindi cha pili na pengine tulistahili kushinda mabao mengi"

"Sare hii waliyoipata sio kwa sababu ya ubora wao lakini pia imechangiwa na makosa katika upande wetu. Tumepoteza nafasi nyingi za wazi kama Baleke na Saido wanefunga nafasi walizopata pengine leo tungekuwa tukizungumza mengine"

"Lakini pia bao la pili walilotufunga lilitokana na makosa ya mlinda lango wetu, hivyo kwa ujumla wake tumeyapokea matokeo haya na tunakwenda kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano nyumbani"

"Tutakwenda kumaliza kazi jijini Dar es salaam, Simba hii sio ya kutolewa na Power Dynamos katika mashindano haya. Tumejua wapi tumekosea katika mchezo wa kwanza hivyo tutakwenda kujisahihisha nyumbani ili tufuzu hatua ya makundi," alisema Ahmed

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea Tanzania leo kujiandaa na mchezo unaofuata kwenye  ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Ijumaa ijayo katika uwanja wa Uhuru

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
1h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
4h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
5h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
5h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
5h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
5h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
6h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →