Yanga - Local

Yanga yatoa shukrani Rwanda

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Sep 2023
Yanga yatoa shukrani Rwanda

Rais wa Yanga SC, Hersi Said ameishukuru nchi ya Rwanda ambayo iliwapokea na kuwahakikishia usalama Wanayanga waliosafiri kwa mamia kushuhudia mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Merrikh ya Sudan ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Pamoja na Yanga kuwa ugenini ndani ya ardhi inayoongozwa na Rais Paul Kagame, lakini ni kama ilikuwa nyumbani tu kutokana idadi kubwa ya mashabiki wao kuijaza Kigali na hata mapokezi waliyoyapata kutoka kwa wenyeji wao

Hersi ambaye kabla ya mchezo alimkabidhi Waziri wa Michezo wa Rwanda Aurore Mimosa Munyangaju jezi maalum ya Rais Kagame, amesema Yanga ilikuwa na wakati mzuri Rwanda na inashukuru kwa ukarimu waliopewa

"Tunashukuru kwa mapokezi tuliyopata hapa Rwanda, kwangu ilikuwa heshima kukabidhi jezi ya Yanga kwa Mheshimiwa Waziri wa Michezo wa Rwanda ikiwa ni zawadi maalumu kwa Mheshimiwa Rais Paul Kagame," alisema Hersi

Aidha Hersi amewashukuru Wanachama na Mashabiki wa Yanga waliosafiri kwa wingi Rwanda kwenda kuishangilia timu yao

Hersi amesema wingi wa Wananchi waliosafiri ni ishara ya imani kubwa ambayo Wananchi wameuoa uongozi wake na watahakikisha wanaendelea kuipambania nembo ya klabu

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’