Simba - Local

Simba yaipania Coastal Union

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Sep 2023
Simba yaipania Coastal Union

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ametamba kuwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakuwa maalum kwa klabu hiyo kusahihisha makosa waliyofanya nchini Zambia na kupelekea wakalazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Alhamisi ya wiki hii Simba itashuka uwanja Uhuru kumenyana na Coastal Union katika mchezo ambao awali ulipaswa kupigwa mwishoni mwa mwezi uliopita

"Mpaka sasa taarifa iliyopo ni kuwa mchezo wetu dhidi ya Coastal Union utapigwa uwanja wa Uhuru, lakini kama kutakuwa na mabadiliko tutatoa taarifa"

"Mchezo huu ni muhimu kwetu kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos"

"Kocha wetu (Robertinho) na wachezaji wetu watatumia mchezo huu kujisahihisha kwa kuhakikisha tunaibuka na ushindi mnono kabla ya mchezo wetu dhidi ya Power Dynamos ambao ni lazima tushinde ili tuweze kutinga makundi ya ligi ya mabingwa," alisema Ahmed

Simba inahitaji ushindi dhidi ya Coastal Union ili kurejea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi ambapo Mashujaa Fc inaongoza ikiwa na alama saba baada ya kucheza mechi tatu

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’