Singida - Local

Kilichomuondoa kocha Singida FG ni hiki

Joel JJ By Joel JJ
19 Sep 2023
Kilichomuondoa kocha Singida FG ni hiki

Wiki mbili zilizopita Klabu ya Singida Fountain Gate ilimtambulisha Ernst Middendorp raia wa Ujerumani kuwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Kocha Hans ambaye alikuwa na timu mwanzo wa msimu

Taarifa iliyotoka leo ni kwamba Mwalimu huyo ameomba kuondoka (ameachia ngazi) siku moja baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Future Stars ya Misri mchezo wa CAF CC

Kocha huyo amefanya mazungumzo nakituo cha habari iDiski Times cha Afrika Kusini na kusema ameamua kuachana na Singida FG kufuatia baadhi ya viongozi kuingilia majukumu yake Kwenye mchezo dhidi ya Future Fc

Middendorp alimpanga Gadiel Michael katika eno la kiungo wa ulinzi na kumuweka benchi Morice Chukwu raia wa Nigeria ambaye ndiye anayecheza nafasi hiyo kitendo kilochowakwaza Mabosi wa Singida FG

Mchezo ukiwa unaendelea alipigiwa simu muda wa mapumziko afanye mabadilikona baadae timu ilipata bao moja Baada ya mchezo msimamo wa Viongozi ukawa kama angepanga vizuri kikosi wangeshinda kwa idadai kubwa ya mabao, viongozi walijitetea kwa hoja ya kwamba mwalimu ni mgeni hivyo hawajui vizuri wachezaji wote

Licha ya uongozi wa Singida FG kudai kuwa kocha huyo amepata dharura na atarejea nchini, kulingana na mahojiano aliyofanya huko Afrika Kusini, ni wazi Middendorp huenda hatarejea Singida FG

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
22m ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
3h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
4h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
4h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
5h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →