Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 21 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Sep 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 21 2023

Borussia Dortmund hawana nia ya kumnunua tena winga wa Manchester United na Uingereza Jadon Sancho, 23. (Bild - kwa Kijerumani)

Liverpool wana hamu ya kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 22, ikiwa mshambiliaji wa Misri Mohamed Salah, 31, ataamua kuhama katika klabu hiyo mwezi Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)

Kiungo wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, hana kipengele cha kuachiliwa katika kandarasi yake mpya, inayowaruhusu The Cottagers kudai ada ya juu iwapo Bayern Munich watawasilisha ombi tena baada ya siku ya makataa ya kuwasilisha ombi hilo kumalizika (Football Insider)

Kipengele cha Tottenham kumnunua kwa mshambuliaji Harry Kane katawatumbukia nyongo nahodha huyo wa Uingereza, 30, akirejea Ligi Kuu ya Uingereza, badala ya kuweka ada ya uhamisho. (Daily Mail)

Kurudi kwa Spurs kuna uwezekano wa kutegemea kama Kane anadhani anaweza kufanya kazi tena na mwenyekiti Daniel Levy (Telegraph)

Manchester City wanaweza kumpata bekiwa Boca Juniors na Argentina Valentin Barco, 19, kwa ada ya takriban pauni milioni 15 mwezi Januari. (Football Insider)

Chelsea wanatazamiwa kupokea dau la £400m kutoka kwa kampuni ya uwekezaji ya Ares Management yenye makao yake Marekani kuelekea uwanja wao mpya na miradi mingine. (Telegraph) Uwekezaji huo pia utasaidia Blues kugeuka kuwa shirika la klabu nyngi na kupunguza gharama ya mishahara huko Stamford Bridge. (Goal)

Spurs wako tayari kumpa mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 31, mkataba mpya wa kuongeza muda wake wa kusalia London kaskazini mwaka wa 2025. (90min)

City pia wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa England chini ya miaka 17 Divine Mukasa, 16, kutoka West Ham. (Fabrizio Romano)

Manchester City ilikataa ofa za mkopo kwa mshambuliaji wa Norway Oscar Bobb mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ajax na Porto. (Telegraph)

Mchezaji wa Paris St-Germain Hugo Ekitike, 21, yuko tayari kupigania mustakabali wake katika klabu ya mabingwa hao wa Ufaransa, lakini mshambuliaji huyo wa Ufaransa anafahamu klabu za Ligi ya Premia ikiwemo Crystal Palace, Brentford, Everton, West Ham United na Wolves vina hamu ya kumsajili. (90 Min)

Huddersfield Town wanatazamiwa kumteua mkufunzi wa zamani wa Sheffield Wednesday Darren Moore, 49, kama meneja wao mpya baada ya kuachana na Neil Warnock. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Italia Vincenzo Montella, 49, anatazamiwa kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Uturuki. (Fabrizio Romano)

Manchester United wanatazamiwa kumzawadia mshambuliaji wa England Joe Hugill, 19, kwa mkataba mpya baada ya maandalizi ya msimu mpya. (Manchester Evening News)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’