Simba, Azam Fc viwanjani Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st September 2023


Simba, Azam Fc viwanjani Ligi Kuu

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo michezo miwili inatarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam

Wekundu wa Msimbazi Simba wanarejea katika mbio za ubingwa msimu huu wakiikaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru saa 10 jioni

Wakati Simba ikiwa inasaka ushindi wake wa tatu msimu huu, hali ni tofauti kwa wapinzani wao Coastal Union ambao wanasaka ushindi wa kwanza

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Uhuru msimu uliopita, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1

Matarajio ya mashabiki wa Simba ni kuona timu yao inaendeleza wimbi la ushindi katika msimu ambao wanautaka ubingwa wa Ligi Kuu

Mchezo mwingine kati ya Azam Fc dhidi ya Singida FG utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex

Azam Fc ilioanza vyema msimu huu kwa ushindi katika mechi mbili zilizopita, inasaka ushindi wa tatu wakati Singida FG wameambulia alama mbili tu katika mechi zao mbili zilizopita hivyo ni mchezo ambao watahitaji ushindi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.