Mshambuliaji wa Simba Jean Baleke jana alifunga mabao matatu 'hat-trik' katika mchezo wa ligi kuu ambao Simba walishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union
Baleke amefikisha mabao matano akiongoza mbio za ufungaji bora baada ya mechi tatu kupigwa
Baleke amepachika bao katika kila mchezo ambao Simba wamecheza kwenye ligi msimu huu
Anafuatiwa na Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye alifunga hat-trik ya kwanza msimu huu katika mchezo dhidi ya Tabora United
Stephane Aziz Ki, Max Nzengeli, Mudathir Yahya wote wa Yanga, Iddi Nado, Prince Dube (Azam Fc), Adam Adam (Mashujaa), Matheo Anthony (Mtibwa Sugar) na John Ben wa Tabora United ni miongoni mwa wachezaji ambao wamepachika mabao mawili msimu huu