Klabu ya Al Merrikh kutoka Sudan inatarajiwa kuwasili nchini leo kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Siku ya Jumamosi Septemba 30, Yanga itachuana na Al Merrikh katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema Merrikh watawasili nchini leo Alasiri na Rwandan Air
Al Merrikh wamekuwa mapema kuonyesha 'wanautaka' mchezo huo licha ya kuwa wako nyuma kwa mabao 2-0 ushindi ambao Yanga waliupata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Rwanda
Jumamosi Yanga itahitaji kushinda au matokeo yoyote ya sare kuweza kutinga hatua ya makundi
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi chao kinaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo huo ambao wamepania kuibuka na ushindi
"Maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya AL Merrikh yanaendelea vizuri, jana tulikuwa na session moja na leo tuna session mbili, asubuhi wachezaji wamefanya mazoezi na pia watafanya jioni"
"Tumezisikia kauli za kocha Al Merrikh anasema Yanga inaogopwa barani Afrika lakini sisi tunamwambia asitutoe kwenye reli, tunamsubiri aje uwanja wa Azam Complex tupambane nae katika mchezo ambao tunajua utakuwa sio rahisi," alisema Kamwe
Kamwe alitangaza viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 50,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-
Pia kutakuwa na tiketi za Royal zinazopatikana kwa Tsh 100,000/-



