Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 28 2023

Joel JJ By Joel JJ
28 Sep 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Septemba 28 2023

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi na Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen wanawania kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti iwapo ataondoka Real Madrid mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Cadena Ser – In Spanish)

Kuna hisia ndani ya Manchester United kwamba uhusiano kati ya meneja Erik ten Hag na winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, hauwezi kurekebishwa. (I) Vilabu vya Saudi Arabia vitaongoza mbio za kumsaka Victor Osimhen mbele ya Real Madrid na Chelsea iwapo mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24 atashinikiza kuondoka Napoli mwezi Januari. (Mail)

Sevilla wamekuwa wakimfuatilia kiungo Hannibal Mejbri, 20, lakini Manchester United wanapanga kufanya mazungumzo ya kandarasi na mchezaji huyo wa kimataifa wa Tunisia hivi karibuni ili kumbakisha Old Trafford. (Fabrizio Romano)

Manchester United pia wanapanga mazungumzo na meneja Erik ten Hag kuhusu mkataba mpya (90Min)

Chelsea wako sokoni kutafuta beki mpya wa kushoto, huku mchezaji wa kimataifa wa Italia wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 25 Federico Dimarco na beki wa AC Milan wa Ufaransa Theo Hernandez, 25, wakiwa kwenye orodha yao fupi. (Calciomercato – In Itali)

Sheffield United wamezungumza na kocha wa zamani Chris Wilder kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Paul Heckingbottom kwa kipindi cha pili cha kuinoa klabu hiyo. (Football Insider) Roma wanafikiria kumnunua mlinzi wa Tottenham, 29, Eric Dier, Januari. (Calciomercato – In Italy)

Hatima ya kifedha ya Everton inaweza kuwa shakani ikiwa uchukuaji wa kampuni ya uwekezaji yenye makao yake makuu nchini Marekani ya 777 Partners hautapitishwa. (Guardian)

777 Partners ina uhakika wa kufaulu mtihani wa wamiliki na wakurugenzi wa Ligi ya Premia, na imeanza mazungumzo na makundi ya mashabiki wa Everton ili kujaribu kupunguza wasiwasi wa wafuasi wake kuhusu pendekezo la kuinunua (I) Newcastle walimaliza mkataba wao wa jezi na mtengenezaji wa jezi Caste mapema kutokana na wasiwasi kuhusu ubora wa bidhaa zao. (Subscription Required)

BBC

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
26m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →