Ijumaa Oktoba 06 2023 nchini Afrika Kusini itafanyika droo ya makundi ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions League) na kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup)
Tanzania kama nchi itawakilishwa na timu mbili (2) za Simba na Yanga
Timu zilizofuzu mapaka sasa makundi ya klabu bingwa Afrika ni 15 ambazo ni Al Ahly (Misri), Wydad (Morocco), Pyramids (Misri), TP Mazembe (DR Congo), Jwaneng Galaxy (Botswana), Petro de Luanda (Angola), Esperance de Tunis (Tunisia), Etoile Saleh (Tunisia) na Medema SC (Ghana)
Nyingine ni Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Yanga SC (Tanzania), Simba SC (Tanzania), FC Nouadhibou (Mauritania), Asec Mimosas (Ivory Coast) na Al Hilal (Sudani)
Bado timu moja tu ambayo itafahamika leo Ila kwa asilimia 90 itakuwa CR Belouzdad ya Algeria kwani walishinda kwa magoli 3-1 ugenini na leo ndio mchezo wa marudiano
Draw hufanyika kwa timu 16 kwa kupangwa kwenye pot 4 ikiwa killa POT kuwa na timu 4 na timu zinapangwa kulingana na msimamo wa klabu kwa msimu mitano
Timu zinazokuwa kwenye Pot moja hazitakutana katika hatua ya makundi lakini timu yoyote inaweza kupangwa dhidi ya tmu yoyote kutoka Pot nyingine
Kwa kuzingatia msimamo wa klabu kwa misimu mitano iliyopita, Simba itakuwa Pot 2 wakati Yanga itakuwa Pot 3, maana yake ni kuwa Simba na Yanga zinaweza kupangwa kundi moja
Pot 1 itakuwa na timu za Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Wydad Athletic na Esperance
Pot 2 itakuwa na timu za Pyramids, Petro Atketico, CR Belouisdad na Simba
Pot 3 itakuwa na timu za TP Mazembe, Asec Mimosas, Al Hilal na Yanga
Pot 4 itakuwa na timu za Etoile Sahel, Jwaneng Galaxy, Fc Nouadhibou na Medeama