Klabu ya Tabora United inayoshiriki Ligi Kuu Bara imefungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya wachezaji wa wawili Emmanuel Lamptey na Collins Gymfi kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hiyo
Wachezaji hao raia wa Ghana walifungua kesi FIFA wakidai malipo ya ada ya usajili (sign on fee) na malimbikizo ya mishahara
Tabora United iltakiwa iwe imewalipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipoletwa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pia limetangaza kuifungia Tabora United kufanya usajili wa ndani mpaka pale itakapomalizana na wachezaji hao



