Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mlinda lango wake namba moja Aishi Manula ameanza mazoezi ya timu
Ni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi minne akiuguza jeraha la nyonga baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini
Manula alipata majeraha hayo mwisho mwa msimu uliopita katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao Simba ilicheza dhidi ya Ihefu Fc uwanja wa Azam Complex
Kipa huyo ambaye pia ni tegemeo katika timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' anaweza kuanda kuonekana uwanjani mapema na pengine mchezo ambao Simba watacheza na Al Ahly kwenye AFL Oktoba 20, anaweza kuwa langoni




