Yanga - Local

Yanga yapania kulipa kisasi Mbarali

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Oct 2023
Yanga yapania kulipa kisasi Mbarali

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kimejipanga kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Highlands Estate huko Mbarali

Yanga ilitua Mbeya usiku wa kuamkia leo kuelekea mchezo huo wa raundi ya nne, Wananchi wana kumbukumbu ya kupoteza alama zote tatu msimu uliopita katika mchezo uliopigwa hapo Highlands Estate

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema licha ya timu yake kutopata muda wa kujiandaa na mchezo huo, wako tayari na watapambana kuhakikisha wanashinda

"Tunashukuru tumefika salama Mbeya, hatukuweza kupata muda mzuri wa kujiandaa kama mnavyojua tumetoka kucheza mchezo wa Kimataifa Jumamosi"

"Tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu na tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu," alisema Gamondi

Gamondi amesema licha ya baadhi ya wachezaji kuwa na majeraha, mazoezi ya mwisho leo yatampa nafasi ya kuamua mchezaji gani atamtumia katika kikosi chake hapo kesho

"Wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali yao iko juu, kuna baadhi ya wachezaji wana majeraha lakini tutajua kwenye mazoezi ya mwisho leo jioni ni wachezaji wapi watakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho"

"Tunafahamu kwamba ni mwanzo wa ligi na kila timu iko kwenye nafasi nzuri na kujaribu kufanya vizuri zaidi inapokutana na bingwa mtetezi, ni sisi sasa kuhakikisha tunaendelea kucheza kwa kiwango cha juu na nina imani tutaendelea kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho"

Yanga ndio vinara wa ligi kuu ya NBC baada ya kushinda mechi zote tatu za mwanzo, ni wazi Wananchi watazihitaji alama tatu hapo kesho ili kuhakikisha wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’