Ihefu Fc yaendeleza ubabe dhidi ya Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th October 2023


Ihefu Fc yaendeleza ubabe dhidi ya Yanga

Tunaweza kusema uwanja wa Highland Estates sio eneo salama kwa Yanga baada ya leo tena kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc kwa kufungwa mabao 2-1

Ni vilevile kama ilivyokuwa msimu uliopita, Pacome Zouzoua aliitanguliza Yanga mapema kwenye dakika ya sita lakini Ihefu Fc wakarejea mchezoni baada ya makosa ya kufanyika kwenye eneo la Yanga

Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto alifanya madhambi karibu na eneo la hatari baada ya kuchelewa kuondoa mpira kwenye eneo la hatari

Mpira wa adhabu kutoka Never Tigere ulimshinda mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra akishindwa kuondosha eneo la hatari na Lenny Kissu kuweka bao kimiani

Bao la pili la Ihefu Fc lilifungwa na Charles Ilanfya baada ya shambulizi la kushitukiza

Huu ni ushindi wa pili kwa Ihefu Fc msimu huu katika mechi nne walizocheza, ukiwa pia ni ushindi wa pili katika uwanja wao wa nyumbani


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.