Wekundu wa Msimbzi Simba Sc wamerudi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida FG katika mchezo uliopigwa uwanja wa LITI
Mabao ya Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri yalitosha kuihakikishia Simba alama tatu muhimu ambazo zimewarejesha juu ya msimamo baada ya kufikisha alama 15
Bao la kufutia machozi kwa upande wa Singida FG lilifungwa na Deus Kaseke
Ni ushindi wa tano mfululizo kwa Simba ambayo kwa hakika imeonyesha dhamira yake, inautaka ubingwa msimu huu
Nayo Tanzania Prisons imezinduka na kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu ikiichapa Mtibwa Sugar mabao 3-2
Prisons wameondoka mkiani mwa msimamo wakichupa mpaka nafasi ya 13 wakifikisha alama 4