Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 09 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 09 2023

AC Milan wamemuongeza mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kwenye orodha rasmi ya makipa wa kikosi chao kufuatia kuokoa muda wake wa kusimama katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Genoa

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alichukua glavu kufuatia kadi nyekundu ya dakika ya 97 kwa kipa Mike Maignan. (442)

Kocha mkuu wa Inter Miami Tata Martino amesema "sijui lolote" kuhusu uvumi unaomhusisha gwiji wa Argentina Lionel Messi, 36, na kuhamia Barcelona kwa mkopo wakati wa mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya Soka, utakaoanza mwishoni mwa Oktoba hadi Februari. (Goal)

Wayne Rooney, 37, yuko mbioni kuwa meneja wa klabu ya Birmingham City baada ya kuacha nafasi yake kama kocha mkuu wa DC United inayoshiriki Ligi ya MLS. (Times)

Rooney atamchukua mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Ashley Cole na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United John O'Shea kwenda nao Birmingham City ikiwa klabu hiyo itaamua kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa sasa John Eustace. (Mirror)

Ajax itajadili mustakabali wa kocha mkuu Maurice Steijn baada ya timu hiyo ya Uholanzi kushuka katika timu tatu za mkiani kwa kushindwa kwa tatu mfululizo kwenye Eredivisie. (Fabrizio Romano)

Aliyekuwa meneja wa Ajax Louis van Gaal, ambaye hivi majuzi alijiunga na bodi ya usimamizi ya klabu hiyo, alikuwa kwenye viti kutazama kichapo chao cha hivi punde - 2-1 nyumbani dhidi ya AZ Alkmaar siku ya Jumapili. (Sport)

Manchester United inawafuatilia kiungo wa Palmeiras Luis Guilherme na winga wa Flamengo Lorran, wote wenye umri wa miaka 17, lakini wanaweza kulazimika kutumia hadi £100m kuwapata vijana hao wa Brazil. (Star)

Sevilla wanatarajia kupata mbadala wa haraka baada ya kumfukuza meneja Jose Luis Mendilibar siku ya Jumapili. Kocha huyo wa Basque aliisaidia Sevilla kushinda taji la saba la Ligi ya Europa msimu uliopita lakini ameiongoza kushinda mara mbili pekee kati ya mechi nane katika kampeni za sasa za La Liga. (AS - In Spanish)

Brentford wanafikiria kumnunua winga wa Sunderland Muingereza Jack Clarke kwa pauni milioni 15 Januari. (Alan Nixon via Chronicle)

Mjerumani Danny Rohl, 34, ambaye amekuwa na majukumu ya ukocha na RB Leipzig, Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, anaibuka kuwa meneja anayefuata Sheffield Wednesday. (Mail)

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Newcastle na Crystal Palace Loic Remy ametangaza kustaafu, akiwa na umri wa miaka 36. Mfaransa huyo amekuwa mchezaji huru tangu aachiliwe na Brest msimu wa joto. (Sun)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’