NIC kutoa tuzo ya mchezaji bora Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th October 2023


NIC kutoa tuzo ya mchezaji bora Yanga

National Insurance Cooperation (NIC) imeingia mkataba na Yanga kwa ajili ya kutoa tuzo za mchezaji bora wa Yanga ambazo zitatolewa kila mwezi

Mkataba huo wa miaka mitatu una thamani ya Tsh Milioni 900

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mkataba huo matokeo mazuri ya uhusiano kati ya Yanga na NIC akiamini utawapa fursa wachezaji wa Yanga kutuzwa katika kila mwezi

"Mkataba huu ni wamiaka mitatu na thamani yake itakuwa milioni 900. Mkataba huu utakuwa unalenga moja kwa moja kwa mchezaji bora wa mwezi,tunakuhakikishia mkataba huu utakupa thamani sahihi ya kile ulichokiwekeza kwetu"

"Kwetu sisi kama Yanga Sc ni heshima kubwa sana kufanya kazi na kampuni kubwa kama hii kutokana na utendaji wetu sahihi ndani ya klabu yetu"

"Tunakuakikishia ushirikiano mkubwa sana toka kwetu na tunakuakikishia tutakwenda mbali zaidi ya hapo sisi na kampuni yako," alisema Hersi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.