Mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney amekubali dili la kuinoa Birmingham City kwa mshahara ambao ni mara tatu zaidi ya John Eustace aliokuwa nao kabla ya kutimuliwa na timu hiyo ya Championship. (Times – Subscription)
Manchester United iko tayari kutoa ruzuku ya mshahara wa winga wa Uingereza Jadon Sancho wa pauni 300,000 kwa wiki ili kumtoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa mkopo mwezi Januari kama ataendelea kukataa kuomba msamaha kwa meneja Erik ten Hag. (Mail)
Mshambulizi wa Brazil Vinicius Jr bado hajasaini mkataba mpya na Real Madrid, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa miaka 23 ukikamilika msimu ujao wa joto. (Sport – In Spanish)
Chelsea itamruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Roma, kuondoka kwa takriban pauni milioni 37 msimu ujao. (Fabrizio Romano)
Sporting Lisbon wanaweza kuchukua hatua ya kumrejesha beki wa Uingereza Eric Dier, 29, katika klabu hiyo mwezi Januari, au mkataba wake utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Times - Subscription Required)
Rais wa heshima wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema klabu hiyo ya Ujerumani ililipa £82m (euro 95m) kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 30, kutoka Tottenham msimu wa joto badala ya £85m (euro 100m) pamoja na nyongeza ambazo zilinukuliwa sana. (BR24)
Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis yuko tayari kuambatana na meneja Mfaransa mwenye presha Rudi Garcia kwa wakati huu, licha ya klabu hiyo kuanza vibaya msimu huu kutetea ubingwa wao wa Serie A. (Soccer Italia)
Meneja wa zamani wa Brighton na Chelsea, Muingereza Graham Potter, ni mmoja kati ya majina matatu, pamoja na Mcroatia Igor Tudor na Muargentina Marcelo Gallardo, ambao Napoli inaweza kuwateua iwapo watachukua nafasi ya Garcia. (Foot Mercato)
Manchester United wako kwenye mazungumzo na beki wa kulia wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 25, kuhusu mkataba mpya. (Football Insider) Manchester United pia wanatafuta kusajili wachezaji wawili wa Kibrazil wenye umri wa miaka 17 - kiungo wa Palmeiras Luis Guilherme na winga wa Flamengo Lorran. (Mirror)
Beki wa Juventus Federico Gatti, 25, ataongeza mkataba wake na klabu hiyo hadi 2028 baada ya kurejea kutoka katika majukumu ya kimataifa na Italia. (Tuttosport, via Tuttomercatoweb) Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone, 53, amekubali kwa mdomo kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uhispania. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United na Uingereza David Beckham, 48, atapewa wadhifa wa ubalozi katika klabu hiyo ya Old Trafford iwapo atachukuliwa na Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani. (talkSPORT).
Klabu ya Ufaransa Bordeaux inataka kumteua winga wa zamani wa Liverpool Albert Riera kama meneja wao mpya - na wako kwenye mazungumzo na NK Celje wa Slovenia ili kumwachilia Mhispania huyo, 41, kutoka kwa mkataba wake nao. (L'Equipe – In French Kifaransa)
BBC