Simba - Local

Manula arejea Simba ikishinda 5-1 mechi ya kirafiki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Oct 2023
Manula arejea Simba ikishinda 5-1 mechi ya kirafiki

Leo Jumamosi asubuhi Simba imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dar City kwenye uwanja wake wa Mo Simba Arena, Bunju - Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1, huku kipa wake Aishi Manula akirejea langoni.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Manula msimu huu kwani kabla ya hapo alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya nyonga aliyoyapata Aprili 7, mwaka huu kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (ASFC), dhidi ya Ihefu katika Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo wa leo, Manula alianza langoni Simba akicheza kwa dakika 40, kabla ya kufanyiwa mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Abel ambaye naye bado hajapata muda wa kutosha kucheza ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe mwanzoni mwa msimu akitokea KMC.

Kurejea kwa Manula ni taarifa njema kwa Simba kuelekea mchezo wa AFL dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Ijumaa, Otoba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Manula huenda akawa tayari kuwakabili Al Ahly katika mchezo huo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’