Singida FG leo imemtambulisha Ricardo Ferreira raia wa Brazil kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo
Ricardo ana uzoefu na soka la Afrika kwani amewahi kuzinoa Al Hilal, Al Merrikh zote za Sudan pamoja na Ismaily ya Misri
Ricardo ametua kuchukua nafasi ya Ernst Middendorp aliyeondoka baada ya kudai kuingiliwa kwenye majukumu yake
Ricardo anaungana na Robertinho Oliveira kuwa kocha wa pili kutoka Brazil kufundisha ligi kuu ya NBC msimu huu



