Barcelona wana nia ya kumsajili mshambulizi wa Manchester United Jadon Sancho mwezi Juni, ikiwa wanaweza kukubaliana na dili la bei iliyopunguzwa. Winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 pia amehusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda Juventus. (Sport - in Spanish)
Mtendaji mkuu wa Inter Milan Giuseppe Marotta amekataa kuondoa uwezekano wa mlinda mlango wa Cameroon Andre Onana, 27, kurejea katika klabu hiyo ya Serie A baada ya kuanza kwa mwendendo usioeleweka Manchester United kufuatia uhamisho wa majira ya joto kutoka San Siro. (Mail)
Bruno Guimaraes, 25, ana kipengele katika mkataba wake mpya wa Newcastle United ambao utamruhusu kiungo huyo wa kati wa Brazil kujiunga na Barcelona kwa ada ya euro 65-70m (£56.4m-£60.7m). (Sport - in Spanish)
Liverpool wamemfanya mshambuliaji wa Ujerumani Leroy Sane, 27, kuwa mlengwa wao namba moja kuchukua nafasi ya Mohamed Salah, 31, ikiwa Mmisri huyo ataondoka na huenda akavunja rekodi yao ya uhamisho ili kumpata nyota huyo wa Bayern Munich. (Mirror)
Mshambulizi wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr, 23, anasema alimtumia ujumbe kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 20, ili kumshawishi abadilike kutoka Borussia Dortmund hadi Bernabeu msimu wa joto. . (L'Equipe - in French)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola alipiga simu kwa saa tatu na Bellingham kabla ya kuhamia Real Madrid kwa nia ya kumshawishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kujiunga na washindi wake mara tatu. (Cadena Ser via Goal)
Kiungo Kalvin Phillips, 27, anafikiria kuhama Manchester City mwezi Januari kwa kuhofia kukosa muda wa kucheza kunaweza kuzuia nafasi yake ya kujiunga na kikosi cha Gareth Southgate Euro 2024. (Mirror)
Aston Villa na Crystal Palace ni miongoni mwa timu za Ligi ya Premia zinazomfuatilia mshambuliaji wa Norwich wa England chini ya umri wa miaka 21 Jon Rowe, 20, ambaye amebakisha miezi 18 katika mkataba wake Carrow Road. (Mail)
Kiungo wa kati wa Uingereza Charlie Patino, 19, anataka kujihakikishia mustakabali wa muda mrefu katika klabu mama Arsenal wakati muda wake wa sasa wa mkopo Swansea utakapomalizika. (Mail)
Barcelona wanajipanga kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea na Uholanzi Ian Maatsen, 21, ambaye alikataa uhamisho wa pauni milioni 32 kwenda Burnley na mkataba wake unamalizika mwezi Juni. (Sport - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Manchester United Scott McTominay, 26, anatazamiwa kusalia katika klabu hiyo kwa muda wote uliosalia, huku meneja Erik ten Hag akifutilia mbali uhamisho wa Januari kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland ambaye alihusishwa na West Ham msimu wa joto. (Star)
BBC



