Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 16 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th October 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 16 2023

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Emile Smith Rowe, 23, ananyatiwa na klabu nyingine ya Ligi Kuu ya Uingereza Newcastle United. (Mirror)

Inter Milan wanahusishwa na kiungo wa West Ham wa Czech Tomas Soucek, 28, na mshambuliaji wa Leicester City wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 27. (FC Inter News - in Italian)

West Ham wanatazamiwa kuimarisha mazungumzo ya kandarasi na Soucek, ambaye anatarajiwa kuwa mchezaji huru msimu ujao. (Football Insider)

Chelsea wako tayari kumuuza mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, mwezi Januari huku mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakimtaka. (Fabrizio Romano, kupitia Goal)

Paris St-Germain watatoa ofa ya mwisho ya kumuongezea mkataba mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, wiki ijayo - ikiwezekana kwa kipengele cha chini cha kuachilia - huku Real Madrid wakisubiri kuona nini kitatokea kwenye majadiliano. (Sport - kwa Kihispania)

Mkufunzi wa Ugiriki Gus Poyet anasema angependa kuinoa Jamhuri ya Ireland wakati fulani, baada ya kuiongoza timu yake kushinda mara mbili dhidi ya Waireland kwenye mechi ya kufuzu kwa Euro 2024. (Irish Independent)

Manchester City wanaweza kupata zaidi ya £8m kwa sababu ya kipengele cha kuuzwa iwapo Liverpool itamsajili winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 27. (Mirror)

Uwekezaji wa 25% wa Jim Ratcliffe katika Manchester United bado haujakamilika na huenda mazungumzo yakachukuwa muda mrefu. (Independent)

Bayern Munich na Barcelona zote zinamtaka kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 20. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Manchester United hawana haraka ya kumuuza kiungo wa Scotland Scott McTominay, 26, lakini watazingatia makubaliano kama bei itakuwa sawa. (90 min)

Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hatakuwa meneja mpya wa Charlotte FC baada ya rais wa timu hiyo Joe LaBue kuandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba raia huyo wa Norway alikuwa akitembelea kituo cha klabu ya MLS pekee. (Manchester Evening News)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.