Mchezo kati ya Ubelgiji na Sweden wa kufuzu EURO 2024 jana usiku haukuendelea baad aya mapumziko kufuatia wachezaji kukataa kujitokeza kucheza kipindi cha pili na mchezo huo kufutwa baada ya mashabiki wawili wa Sweden kupigwa risasi na kufariki katika Jiji la Brussels mji mkuu wa Ubelgiji
Imeelezwa lilikuwa shambulizi la kigaidi ambapo mhalifu huyo alifanya tukio hilo karibu na uwanja
Bada ya mchezo kuahirishwa mashabiki wa Sweden walisindikizwa na Polisi hadi mahali salama huku wa Ubelgiji wakirejea majumbani
Aidha wachezaji wa Sweden wao walisindikizwa uwanja wa ndege kurejea nchini kwao
Wakati uamuzi wa kusimamisha mchezo unachukuliwa matokeo yalikuwa Ubelgiji 1- 1 Sweden
UEFA imethibitisha kuahirishwa kwa mchezo huo baada ya kushauriana na timu zote mbili na kwamba watafanya mawasiliano kwa wakati unaofaa.