Newcastle United wanatayarisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 27. (Mail)
Bayern Munich pia wamezungumza na City kuhusu hali ya Phillips, lakini kiungo wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, anasalia kuwa mlengwa mkuu wa klabu hiyo ya Ujerumani. (90 min)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco amewasiliana na mawakala wa Frenkie de Jong kujadili mpango wa kurefusha kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, lakini kiungo huyo kimataifa wa Uholanzi hana haraka ya kuanza mazungumzo. (Sport - kwa Kihispania)
Deco anasema itakuwa vigumu kwa Barcelona kuongeza wachezajiwapya kwenye kikosi chao wakati wa usajili wa Januari kwa sababu ya hali ya kifedha ya klabu hiyo. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ligi ya Premia zinazomsaka mshambuliaji wa Ujerumani Jamal Musiala, 20, ambaye mkataba wake na Bayern Munich utaendelea hadi 2026. (Sport Bild - kwa Kijerumani)
Liverpool ilituma maskauti kumtazama mlinzi wa Ureno na Sporting Goncalo Inacio, 22, wakati wa mechi ya nchi yake dhidi ya Bosnia-Herzegovina. (90 min)
Kikosi cha Jurgen Klopp pia ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ligi Kuu ya Uingereza zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa Schalke Assan Ouedraogo, 17. (Sky Sports Germany).
Mwekezaji mpya mtarajiwa wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe alitilia shaka kuajiriwa kwa klabu hiyo ilipotembelea Old Trafford mwezi Machi, akitumia ununuzi wa kiungo wa Brazil Casemiro, 31, kutoka Real Madrid mnamo Agosti 2022 kama mfano. (Guardian)
Ununuzi wa Ratcliffe wa asilimia 25 ya United hautarajiwi kupigiwa kura na bodi yao siku ya Alhamisi huku maelezo ya mwisho ya mkataba huo yakitatuliwa. (Telegraph - usajili unahitajika)
Beki wa Manchester United na Uswidi Victor Lindelof, 29, anatarajia klabu hiyo itazingatia kipengele cha kuongeza mwaka mmoja katika mkataba wake zikiwa zimesalia miezi 12 katika mkataba wake wa sasa. (90 min)
Beki wa Mashetani Wekundu na Ireland Kaskazini Jonny Evans, 35, amesema alihofia angelazimika kustaafu soka kwa sababu ya majeraha msimu uliopita kabla ya kurejea Manchester msimu wa joto. (90 min)
Aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kuajiri wa Tottenham Paul Mitchell anapendekezwa kuwa mkurugenzi mpya wa kandanda katika klabu ya Manchester United, jambo ambalo linaweka kazi ya mkurugenzi wa sasa wa kandanda John Murtough hatarini. (The I)
BBC