Al Ahly watua usiku tayari kuikabili Simba AFL

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th October 2023


Al Ahly watua usiku tayari kuikabili Simba AFL

Wapinzani wa Simba kwenye mchezo wa African Football League, Al Ahly wamewasili nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea mtanange huo wa kukata na shoka ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Wakati Al Ahly wakitua, kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake Mo Simba Arena kuelekea mchezo huo

Leo majira ya saa 10:15 jioni Simba itafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa

Wapinzani wao Al Ahly watafanya mazoezi dimba la Mkapa saa 12, muda ambao mchezo huo utapigwa

Wageni kutoka mataifa mbalimbali wameendelewa kuwasili nchini kushuhudia historia ikiandikwa katika uzinduzi wa African Football League


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.