Simba vs Al Ahly, VAR kutumika

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th October 2023


Simba vs Al Ahly, VAR kutumika

Mtanange wa ufunguzi African Football League kati ya Simba dhidi ya Al Ahly utapigwa saa 12 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Teknolojia ya usaidizi wa waamuzi kwa video (VAR) itatumika leo katika mchezo huo mkondo wa kwanza robo fainali 

Hii ni michuano mikubwa yenye sura ya kidunia, inasimamiwa na FIFA, haishangazi kuona VAR inatumika

Maafisa waandamizi wa FIFA wakiongoza na Rais Gianni Infantino pamoja na kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao watakuwa dimba la Mkapa leo kushuhudia ufunguzi

Patrice Motsepe ambaye ni Rais wa CAF, yeye ataongoza jopo la waandamizi kutoka CAF

Leo majira ya mchana Motsepe atazungumza na wanahabari kuweka hadharani kombe ambalo bingwa wa michuano hii atakabidhiwa

Kwa hakika hii ni siku kubwa kwa klabu ya Simba na Watanzania kwa ujumla


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.