Kocha Azam Fc atamba, amepata dawa ya Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st October 2023

Kocha Azam Fc atamba, amepata dawa ya Yanga

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amewaambia wachezaji wake kuonesha thamani yao ya juu katika kila mchezo ukiwemo wa dhidi ya Young Africans utakaopigwa Jumatatu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam

Dabo amesema anawafahamu Young Africans kwa kuwa alikutana nao kwenye mechi ya Ngao ya Jamii na kufungwa mabao 2-0 lakini anaamini hii ni mechi nyingine na amewaandaa wachezaji wake kwa namna nyingine

"Nimewaeleza wachezaji wangu tangu tumeanza msimu kwamba hatuchezi na mpinzani mmoja au wawili, tunapaswa kucheza vizuri kila wakati, kupambana na kuonesha thamani yetu kwa kushikamana na utayari kila mchezo, hilo ndio la muhimu"

"Na sasa tunakutana na Young Africans, timu ambayo tulikutana nayo Tanga (Uwanja wa Mkwakwani) katika Ngao ya Jamii, ulikuwa wakati mzuri kuwafahamu lakini huu ni mchezo mwingine na kuna utofauti tangu wakati ule na sasa hivyo tunaendelea kujiandaa tukitazamia kukua zaidi kila wakati," amesema Dabo raia wa Senegal.

Timu hizo zinakutana wakati Azam ikiwa juu kwenye nafasi ya pili kwa pointi 13 baada ya ushindi wa medhi nne na sare moja, huku Young Africans ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 12 ilizovuna baada ya ushindi wa mechi nne na kufungwa mchezo mmoja.

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’