Msafara wa kikosi cha Simba uliwasili nchini Misri majira ya usiku wa kuamkia leo kuelekea mchezo wa mkondo wa pili robo fainali AFL dhidi ya Al Ahly
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumanne nchini humo. Simba ilisafiri na msafara wa wachezaji 24 nchini Misri kuisaka nafasi ya kutinga nusu fainali dhidi ya mabingwa hao wa Afrika
Katika mchezo huo Simba itahitaji ushindi au matokeo ya sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kutinga nusu fainali
Sare ya mabao 2-2 itapelekea mchezo huo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati




