Azam - Yanga - Local

Azam Fc kufuta uteja dhidi ya Yanga leo?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Oct 2023
Azam Fc kufuta uteja dhidi ya Yanga leo?

Wakati Azam ikiwa mgeni wa Yanga leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kocha wa kikosi hicho, Youssouph Dabo amesema licha ya ugumu uliopo ila sababu itakayowapa ushindi ni nidhamu kwa wachezaji kuanzia kujilinda hadi ushambuliaji

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dabo amesema Yanga ni timu bora ambayo wanaiheshimu kwa kiasi kikubwa, lakini wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara katika msimu huu

"Sio rahisi unapocheza na timu kama Yanga kwa sababu ina wachezaji wazuri ambao tayari wameonyesha ubora mkubwa msimu huu, hivyo kwetu ni kipimo sahihi cha kuonyesha ni kwa jinsi gani tunahitaji kufikia malengo tuliyojiwekea," alisema Dabo

Dabo amesema kitendo cha mchezo huo kuondolewa katika Uwanja wa Azam Complex na kuhamishiwa Benjamin Mkapa hakitawaathiri wachezaji wa timu hiyo licha ya kuzoea mazingira ya nyumbani ambako ndiko wamekuwa na matokeo mazuri kwa asilimia 100

"Kama nilivyosema mwanzoni huu mchezo haujalishi unachezea wapi kwa sababu tunakutana na timu bora. Jambo la msingi na la muhimu ni maandalizi mazuri ya kiuchezaji kwa maana ya kucheza kwa tahadhari ya kujilinda na kutumia vizuri nafasi"

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa Agosti 9, mwaka huu katika Ngao la Jamii ambapo Azam ilipoteza mabao 2-0 huku kwenye Ligi Kuu Bara ikifungwa 3-2, Desemba 25 mwaka jana, mechi iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’