Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 23 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Oktoba 23 2023

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 31, huenda asipewe ofa ya kuongezewa kandarasi katika klabu ya Manchester City iwapo rekodi yake ya jeraha itazidi kuwa mbaya. (Football Insider)

Arsenal wanatafuta kumnunua kiungo wa kati wa Fluminense Mbrazil Andre, 22, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Fichajes – In Spanish)

Manchester City inachunguza uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala, huku Liverpool pia wakimpenda kwa muda mrefu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Football Insider)

Mshambulizi wa Inter Miami Muargentina Lionel Messi, 36, hafikirii mkataba wowote wa mkopo kuanzia sasa hadi msimu mpya wa MLS uanze mwezi Februari licha ya kuhusishwa na Barcelona. (Fabrizio Romano)

Chelsea wanaendelea kufuatilia kwa ufupi hali ya fowadi wa Nigeria Victor Osimhen inayoendelea Napoli, licha ya tetesi za kuhamia Liverpool kuafikiwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (TeamTalk)

Beki wa kushoto wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies atagharimu Real Madrid angalau pauni milioni 40 ikiwa klabu hiyo ya La Liga inataka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Bild)

Luton italazimika kulipa angalau pauni milioni 5.5 kwa kiungo wa Ecuador mwenye umri wa miaka 19 Oscar Zambrano huku klabu yake ya LDU Quito ikishikilia ofa bora zaidi. (Sun) Rangers wangetaka ofa za angalau £5m ili kumuuza kipa wao Muingereza Jack Butland, 30. (TeamTalk)

Beki wa zamani wa Spurs Cameron Carter-Vickers, 25, hana haraka ya kurejea Ligi ya Premia, huku Mmarekani huyo, ambaye kwa sasa yuko Celtic, akiendelea kuzua gumzo la uhamisho. (Goal)

Fluminense ya Brazil inajiandaa kumnunua mlinzi wa Chelsea Thiago Silva huku kukiwa na uvumi kwamba Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 39 ataondoka Stamford Bridge mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes – In Spanish)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’