Al Ahly chupuchupu mbele ya Simba Misri

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th October 2023


Al Ahly chupuchupu mbele ya Simba Misri

Simba imeondoshwa kwenye michuano ya African Football League kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly katika mchezo uliopigwa huko Misri leo

Moja ya mechi bora kabisa kwa kocha Robertinho Oliveira ambaye alikuja na mbinu sahihi za kuwadhibiti Al Ahly katika uwanja wao wa nyumbani

Bao la Sadio Kanoute nusura liifanye Simba irejee historia yake ya mwaka 2003 kwa kuwatoa vigogo wengine wa Misri katika mashindano

Lakini Mohammed Karhaba aliwanusuru Al Ahly na kipigo akisawazisha kwenye dakika ya 75

Mabao ya ugenini yameibeba Al Ahly kwani mchezo huo umemalizika kwa sare ya mabao 3-3 lakini Al Ahly wamefaidika kwa sababu walifunga mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza

Lakini habari kubwa ni kile alichofanya Simba katika uwanja wa KImataifa wa Cairo. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Simba iko karibu sana kufikia malengo yake ya kulitawala soka la Afrika

Al Ahly ni mabingwa wa Afrika, timu bora ya karne lakini leo walihitaji bahati na kumuomba mungu kufanikiwa kuvuka mbele ya Mnyama

Hongera kwa wachezaji na hongera kwa benchi la ufundi, huyu Robertinho imefika wakati Wanasimba wanapaswa kumuheshimu kwani ataifikisha Simba mbali sana


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.