Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya African Football League, kikosi cha Simba kimerejea kutoka Misri mchana wa leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema sasa nguvu zote wanazihamishia kwenye mechi zinazofuata katika ligi kuu ya NBC
Mchezo dhidi ya Ihefu Fc ndio unaofuata kwenye ratiba ambapo Jumamosi, Oktoba 28 Simba itashuka uwanja wa Mkapa kumenyana na walima mpunga hao kutoka Mbarali
Ahmed amesema mkakati wa Simba ni kuendelea kugawa vipigo kwa kila timu inayokuja mbele yao
Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa Jumamosi katika mchezo huo ambao wamedhamiria kutoa adhabu kali kwa Ihefu Fc
"Sasa focus ni kwenye ligi kuu ya NBC, Tuendelee kugawa dozi kila anaekuja mbele yetu Wana Lunyasi tuanze sasa kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Wababe wao Jumamosi ya October 28 Benjamini Mkapa," alitamba Ahmed
Baada ya mchezo huo, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Yanga, utapigwa Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa