Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zimethibitisha kuwa mlinda lango Metacha Mnata bado hajarejea kunako kikosi hicho baada ya Kocha Miguel Gamondi 'kumuwekea ngumu' kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa
Tangu atue Yanga, Gamondi ameonekana kuwa na msimamo kwenye masuala ya nidhamu ya wachezaji kama alivyokuwa mtangulizi wake Nasreddine Nabi
Metacha alichelewa kujiunga na kikosi cha Yanga baada ya majukumu ya timu ya Taifa na alitakiwa kutoa maelezo kwani hakutoa sababu mapema kwa nini amechelewa
Kwa sasa bado hayuko sehemu ya kikosi akikosa mechi tatu zilizopita kwenye ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc, Geita Gold na Azam Fc
Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery ndio walinda lango wanaoonekana kwenye mazoezi ya Yanga pale Avic Town