Coastal Union yazinduka Tanga, yaichapa Mashujaa 2-0

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th October 2023


Coastal Union yazinduka Tanga, yaichapa Mashujaa 2-0

Wagosi wa Kaya Coastal Union wamezinduka katika uwanja wa nyumbani, Mkwakwani wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Mabao ya Bakari Selemani na Lucas Kikoti (p) yaliihakikishia Coastal Union ushindi wao wa kwanza msimu huu

Coastal Union wangeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi wakipoteza nafasi nyingine kupitia mkwaju wa penati

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Coastal Union msimu huu pia wakifunga kwenye uwanja wa nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu

Mashujaa Fc iliyoanza vyema msimu, leo imepoteza mchezo wa pili mfululizo

Aidha JKT Tanzania nayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex mapema

Bao pekee la JKT Tanzania lilifungwa na Maka Edward kwenye dakika ya 17


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.