Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Oktoba 26 2023

Joel JJ By Joel JJ
26 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Oktoba 26 2023

Manchester United wabadili msimamo na kumtaka David de Gea arejee kwa mkataba wa muda mfupi - miezi minne baada ya kumruhusu mlinda lango huyo wa zamani wa Uhispania, 32, kuondoka mwishoni mwa kandarasi yake. (Sun) Manchester City inachunguza uwezekano wa kumsajili winga wa Bayern Munich Jamal Musiala, 20. (Sport - in Spanish)

Washindi hao wa Treble msimu uliopita watakabiliana na ushindani kutoka kwa Liverpool kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Bild)

Bayern haina uhakika kuhusu kutafuta ofa ya kumnunua Joao Palhinha wa Fulham mwezi Januari baada ya kukaribia kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ureno, 28, msimu uliopita. (Bild)

Manchester United na Liverpool wamekuwa wakimtazama beki wa Uhispania Robin le Normand, 26, na wanaweza kumsajili kutoka Real Sociedad mwaka ujao. (Team Talks)

Aston Villa wameibuka kuwa mstari wa mbele kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid Nahuel Molina, 25, ambaye aliisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia mwaka jana. (Fichajes – In Spanish)

Kocha wa Ureno Jose Mourinho anatarajiwa kuondoka Roma mwishoni mwa msimu huu na mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 26, anaweza kumfuata nyuma kwenye Ligi ya Premia. (Team Talks)

West Ham wanaweza kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Club America na Uruguay Sebastian Caceres, 24, mwezi Januari kwa kitita cha £6m. (Football Insider)

Manchester United, Arsenal na Manchester City wanaendelea kumfuatilia Michael Kayode licha ya beki huyo wa kulia wa Italia, 19, kutia saini mkataba mpya Fiorentina. (90min)

Ian Maatsen anatarajiwa kuondoka Chelsea mwezi Januari baada ya kushindwa kupata nafasi ya kuanza, lakini Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye anacheza nafasi ya beki wa kushoto au kiungo, hana nia ya kurejea Burnley, ambako alikaa msimu uliopita kwa mkopo. (Team Talks)

West Ham wako tayari kuanza kutafuta mbadala wa meneja David Moyes. (Football Insider)

Beki wa zamani wa Ugiriki Sokratis Papastathopoulos, 35, anatazamiwa kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal Hector Bellerin huko Real Betis akiwa mchezaji huru tangu aondoke Olympiakos. (Fabrizio Romano)

Beki wa zamani wa Barcelona na Mexico Rafael Marquez yuko tayari kukifundisha kikosi cha kwanza cha Barca baada ya kuonesha kiwango kizuri akiwa na kikosi B cha klabu hiyo, anasema mchezaji mwenzake wa zamani Gerard Pique. (ESPN)

Mshambulizi wa Al-Nassr na Senegal Sadio Mane, 31, yuko katika harakati za kuinunua klabu ya daraja la nne ya Ufaransa Bourges Foot 18. (ESPN)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
52m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →