Ligi Kuu Bara leo inaendelea tena katika viwanja vitatu hapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga itaikaribisha Singida Big Stars mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkapa saa 12:15
Azam watakuwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Namungo saa 2:30
Mchezo wa mapema utshuhudia KMC ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru
Yanga inayoongoza ligi ikiwa na alama 15 sawa na Simba iliyo na mchezo mmoja wa kiporo, ushindi dhidi ya Singida BS utawahakikishia kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo
Kama Yanga watapoteza mchezo dhidi ya Singida BS na Azam Fc kushinda dhidi ya Namungo, kutakuwa na mabadiliko pale juu ya msimamo Azam Fc anaweza kukaa kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Ihefu Fc hapo kesho
Namungo inasaka ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu Cedric Kaze aliyejiuzulu kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya



