Liverpool na Chelsea wako macho baada ya tetesi kuibuka kwamba mazungumzo ya kandarasi kati ya Napoli na mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, yamekwama. (Mirror)
Mshambuliajii wa Roma Tammy Abraham, 26, atakuwa na hamu ya kurejea Ligi ya Premia ikiwa meneja Jose Mourinho ataondoka katika klabu hiyo ya Italia mwishoni mwa msimu huu, huku Chelsea, Aston Villa na Brentford wakiwa tayari wamearifiwa kuhusu msimamo wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Teamtalk)
Newcastle na Tottenham zote zinamfuatilia fowadi wa Italia Enrico Chiesa na zinaweza kuwashawishi Juventus kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, 26, ambaye mkataba wake unamalizika 2025, kwa dau la euro 60m (£52m) msimu ujao. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Chelsea na Brentford wanamfuatilia mshambuliaji wa Charlton Muingereza Miles Leaburn, 19, ambaye amefungia timu hiyo ya League One mabao sita katika mechi 10 msimu huu. (Daily Mail)
Newcastle wamemjumuisha kiungo wa zamani wa Manchester United Mbrazil Fred, 30, ambaye sasa anachezea Fenerbahce ya Uturuki, kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali ambaye amefungiwa kwa miezi 10 kwa makosa ya kucheza kamari. (Fotomac - kwa Kituruki)
West Ham wako tayari kutoa euro milioni 40 kwa ajili ya kiungo wa Juventus na Italia Manuel Locatelli, 25. (Tutto Juve).
Feyenoord inatarajiwa kudai ada ya takriban euro milioni 100 kwa mshambuliaji wa Mexico Santiago Gimenez, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid, Tottenham, Arsenal na Chelsea. (90 Min)
Arsenal wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa NK Kustosija mwenye umri wa miaka 16 Dino Klapija. Manchester United, Chelsea, RB Leipzig na Borussia Dortmund pia wameonyesha nia ya kumnunua kijana huyo ambaye amewakilisha Croatia na Marekani katika ngazi ya vijana. (Daily Mail)
Arsenal hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa Douglas Luiz Januari mwakani, badala yake watasubiri hadi msimu wa joto kuwasilisha dau la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)
Brentford wanafikiria kuwasilisha ombi la Januari kwa ajili ya kiungo wa kati wa Celtic na Denmark mwenye umri wa chini ya miaka 21, Matt O'Riley, 22. (Teamtalk)
BBC



