Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Oktob 29 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Oct 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Oktob 29 2023

Manchester City wameweka dau la £50m kwa kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, na wamedhamiria kupata faida kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 baada ya kulipa Leeds United £42m mwaka wa 2022. (Mirror)

Vilabu kutoka Saudi Arabia vinapanga kumpa kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin De Bruyne, 32, kitita kikubwa cha mshahara mwaka wa 2024. (Football Insider)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka kiungo wa kati wa Real Sociedad Mhispania Martin Zubimendi, 24, huku mchezaji wa kimataifa wa Real Madrid na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 23, pia akiwavutia. (Mirror)

Tottenham wanavutiwa na mlinzi wa Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 26 Ko Itakura. (Fichajes - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Al-Hilal Ruben Neves, 26, "ana ndoto" za kupata uhamisho wa Januari hadi Newcastle United, ambayo itamlenga mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno baada ya kuthibitishwa kwa marufuku ya Sandro Tonali ya miezi 10. (O Jogo via Sporting witness)

Newcastle watachukua nafasi ya Tonali kwa kusajiliwa kwa mkopo katikati ya mwezi Januari, huku mchezaji wa kimataifa wa Ureno wa Fulham mwenye umri wa miaka 28 Joao Palhinha, Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 22, na kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland Scott McTominay, 26, wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaozingatiwa (Football Insider)

Manchester City na Liverpool wanafuatilia hali ya mshambuliaji wa Bayern Munich Mjerumani Jamal Musiala, 20, ambaye atashinikiza kuhama Januari ikiwa hatapata muda wa kutosha wa kucheza. (Football Insider)

City pia bado wanavutiwa na kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Mfaransa Warren Zaire-Emery, 17. (Sport Zone, kupitia TeamTalk)

Mipango ya Arsenal ya uhamisho wa Januari inaweza kutegemea ukubwa wa jeraha alilopata mshambuliaji wa Wolves na Ureno Pedro Neto katika mchezo wa timu yake dhidi ya Newcastle Jumamosi. (Soka London)

The Gunners watafikiria kumwita winga wa Brazil Marquinhos, 20, kutoka kwa kwenyeMipango ya Arsenal ya uhamisho wa Januari inaweza kutegemea ukubwa wa jeraha alilopata mshambuliaji wa Wolves na Ureno Pedro Neto katika mchezo wa timu yake dhidi ya Newcastle Jumamosi. (Soka.London)

The Gunners watafikiria kumwita winga wa Brazil Marquinhos, 20, kutoka kwenye mkopo wake huko Nantes mwezi Januari. (Mirror)

Mshambulizi wa Nigeria Victor Osimhen, 24, amepuuza mapendekezo kwamba ana nia ya kuondoka Napoli huku kukiwa na ripoti ya kutakiwa Liverpool. (Mirror)

Andrea Pirlo anakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya kushindwa tena kwa timu yake ya Sampdoria kwenye Serie B, huku meneja wa zamani Marco Giampaolo akizingatiwa kuwa mbadala wake. (Calciomercato)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’