Yanga - Local

Yanga livyopania kuvunja rekodi ya mabao

Joel JJ By Joel JJ
30 Oct 2023
Yanga livyopania kuvunja rekodi ya mabao

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI amesema anaiona timu hiyo ikifunga idadi kubwa ya mabao msimu huu tofauti na msimu uliopita kutokana na kutokumtegemea mchezaji mmoja

Yanga hadi sasa ina mabao 20 kati ya hayo ni matatu tu yamefungwa na nafasi tofauti na kiungo ambayo ni bao la Dickson Job, Keneddy Musonda na Hafiz Konkoni mengine yote yamefungwa na viungo.

Aziz Ki amesema kocha Miguel Gamondi ametengeneza timu ya ushirikiano na kuhakikisha inatafuta pointi tatu muhimu bila kujali nani atafunga siku hiyo

"Yanga ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kuona goli hivyo kila anayepata nafasi ya kucheza anaingia uwanjani akiwa na akili ya kuipambania timu kupata matokeo mazuri apambane kufunga na kuzuia hili kwa asilimia kubwa limefanikiwa"

"Naweza nikakosa nafasi ya kufunga akafunga Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Clement Mzize, ukiangalia hadi mabeki wanafunga, hivyo kazi yao sio kulinda tu wanatakiwa kupanda kutengeneza mashambulizi pia wakipata nafasi wafunge kama ilivyo kwa Job," amesema KI

Aziz Ki amesema umoja walioutengeneza ndio siri kubwa ya kucheza kwa kujiamini na kutumia vizuri nafasi wanazozipata akikiri kuwa msimu uliopita haikuwa hivyo kwasababu walikuwa wanaamini katika kumtengenezea nafasi mshambuliaji tu.

Amesema Gamondi amewapa akili kubwa ambayo inawatesa wapinzani wao kila wanapokutana kwani wakimkaba yeye kwa kuamini kuwa ndiye atakayewaadhibu anafunga mchezaji mwingine ambaye hawajamtarajia.

"Hakuna raha ya kucheza mpira bila presha kutoka kwa wapinzani kama ilivyo Yanga ya sasa tunafanya kile ambacho tunaelekezwa na kocha na kimekuwa kikitulipa ubora wetu ni kutokana na kutokujipa umuhimu tunapokuwa uwanjani kila mmoja anachukuliwa kujua anachokifanya uwanjani"

Aziz KI ambaye ametupia mabao sita hadi sasa kwenye mechi saba amesema malengo yao ni kutetea ubingwa na kufunga idadi kubwa ya mabao ili kujenga mwendelezo mzuri eneo hilo ambalo amekiri kuwa na mastaa wengi wenye uwezo

Mabao 20 ya Yanga yamefungwa na Job, Hafiz, Yao, Musonda wote bao moja moja, Pacome (3), Aziz Ki (6), Mudathir (2), Maxi Nzengeli (5).

Yanga itakutana na watani zao Simba, iikiwa imekusanya pointi 18 sawa na Simba ambayo ipo nyuma kwa mchezo mmoja

Mwanaspoti

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
26m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →